Mahakama Kuu ya Venezuela imetoa uamuzi kwamba Delcy Rodrígo ambaye amekuwa akihudumu kama makamu wa rais wa Maduro, achukue nafasi ya rais wa muda katika kipindi hiki chenye kutarajia mabadiliko.
Mahakama kuu inasema kumweka Rodrígo katika nafasi hiyo ni muhimu “ili kuhakikisha mwendelezo wa utawala na ulinzi kamili wa Taifa”.
Mahakama itajadili suala hilo ili “kuamua mfumo wa kisheria unaotumika ili kuhakikisha mwendelezo wa serikali, utawala wa serikali, na ulinzi wa eneo lililo huru katika kipindi ambapo Rais wa Jamhuri amelazimika kutokuwepo”.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “ana wasiwasi mkubwa” na operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela, akiongeza kuwa ina “athari za kutia wasiwasi kwa eneo hilo”