#HABARI: Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imetangaza kuanza kwa mchakato wa awamu mpya ya kampeni kabambe ya msaada wa kisheria maarufu kama “Mama Samia Legal Aid Campaign” mwezi huu wa Januari, huku ikiahidi kufika katika halmashauri na wilaya zote za mkoa wa Morogoro.
Akizungumza leo Jumatatu, Januari 5, 2026, wakati wa ufunguzi wa kliniki ya siku mbili ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro, Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera, amesema kuwa uamuzi wa kuifikia Morogoro kwa mapana zaidi unatokana na uhitaji mkubwa wa huduma hizo katika mkoa huo.
Amesisitiza kuwa huduma hizo zinatolewa bure kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafuta gharama zote ili kuhakikisha Watanzania wanyonge wanapata haki kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa, kata hadi taifa. Katika utekelezaji huo, Wizara itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), mawakili wa serikali, na Jeshi la Polisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.