Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, amezungumzia matukio yaliyotokea mwaka 2025 na kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulinda tunu ya amani huku akiwataka watanzania kuzidisha maombi ili changamoto zilizotokea mwaka uliopita zisijirudie tena ambapo pia amempongeza Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt.Hussein Mwinyi na wananchi wa visiwa hivyo kumaliza uchaguzi mkuu kwa amani na salama.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji na Makazi ya Askari lililopo wilayani Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *