#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuyapa kipaumbele makosa ya uhalifu wa mitandaoni pamoja na makosa ya barabarani yanayosababishwa na madereva wa bodaboda.
Waziri Simbachawene amesisitiza utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, la kuondolewa kwa pikipiki zilizokaa vituoni kwa muda mrefu baada ya wamiliki wake kukidhi masharti ya kisheria kuruhusiwa kuondoka.
Waziri Simbachawene amebainisha hayo wakati akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar, ambapo pia amelitaka jeshi hilo kuendelea kudhibiti vitendo vyote vinavyohatarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.