Shirikisho la vyombo vya habari vya kimataifa limeikosoa serikali ya Israel kwa kuendelea kutekeleza makataa ya kivizuia vyombo vya Habari kufika kwenye eneo la Gaza, shirikisho hilo likiitaja hatua hiyo kuwa yakusikitisha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Serikali ya Israel siku ya jumapili iliiambia Mahakama ya Juu kwamba marufuku hiyo bado itasalia na kutaja hatua hiyo ni kutokana na hatari za kiusalama zinazoendelea katika eneo la Gaza .
Taarifa hiyo iliwasilishwa kujibu ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanahabari wa Kigeni (FPA), ambacho kinawakilisha mamia ya waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini Israel na maeneo ya Palestina.
Tangu vita vya Gaza vilipozuka Oktoba 2023, kufuatia shambulio la Hamas, waandishi wa habari wa kigeni wamezuiwa kuingia katika eneo hilo ingawa Wachache tu ndio wameruhusiwa chini ya uagalizi wa jeshi la Israel.

Chama hicho kiliwasilisha ombi kwa mahakama kwa mara ya kwanza mwaka wa 2024, lakini serikali ya Israel imekuwa ikiongeza muda mara kadhaa kabla ya mahakama hiyo kuweka tarehe 4 Januari kama tarehe ya mwisho ya kusikilizwa kwa ombi hilo.
Mahakama hiyo ya Juu inatarajiwa kutoa uamuzi siku zijazo bila kutaja tarehe rasmi.