Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa usiku wa kuamkia leo yamewalazimu wananchi wa kijiji cha Ntinga, kata ya Msangano wilayani Momba mkoani Songwe kuyakimbia makazi yao.
Maji yaliyovamia nyumba yameharibu vyakula na kusababisha baadhi ya wakazi kukosa hifadhi ya kulala.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, ametembelea eneo hilo na kusema Serikali imeanza kuchukua hatua za dharura na kufanya tathmini ya uharibifu.