Serikali iko mbioni kukamilisha mradi mkubwa wa ‘umeme jua’ ulioopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambao unatarajiwa kuchangia megawati 50 katika gridi ya taifa.
Mradi huo ambao umefikia zaidi ya asilimia 89 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Januari hii huku nyongeza hiyo ya umeme ikitarajiwa kuwanufasha zaidi ya wakazi milioni 2 wa mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani.
Kauli ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba wakati wa kukagua miradi ya umeme ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli kwenda mkoani Simiyu, mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli na mradi huo wa umeme jua.
Mhariri @moseskwindi