VIKOSI vya Ulinzi na Usalama vya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi Vya Idara Maalimu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Pamoja vimefanya Matembezi Maalumu ya Kuadhimisha kutimia Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Matembezi hayo ya Pamoja ya Kuezi Mapinduzi yaliofanyika katika Viunga Mbali mbali Vya Mji wa Zanzibar yaliongozwa na Wakuu wa Vikosi hivyo.