Kampuni ya Azam Marine leo inatarajia kuzindua rasmi boti yake mpya na ya kisasa ya Kilimanjaro IX, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuboresha huduma za usafiri wa baharini nchini.
Boti hiyo, iliyojengwa nchini China kwa kipindi cha miezi 15, ina urefu wa mita 53, ina injini zenye nguvu ya horsepower 8,000 na uwezo wa kubeba abiria 631 kwa wakati mmoja.
Tayari imewasili katika Bandari ya Zanzibar ikiwa imeletwa na meli ya kampuni ya BBC Chartering kwa ajili ya kushushwa na kuanza taratibu za uingizwaji katika huduma.
Kwa mujibu wa Azam Marine, ujio wa Kilimanjaro IX unalenga kuongeza ufanisi, kasi na faraja kwa abiria wanaosafiri kupitia njia zake kuu zinazounganisha Dar es Salaam – Zanzibar – Pemba – Tanga.
✍ Mtumwa Saidi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates