#HABARI: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameuweka wazi mpango wake kumuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kiasi cha hadi Shilingi bilioni mbili kwa ajili ya mikopo ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya vijana waliojiajiri kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni na mitandao ya kijamii.
Akizungumza leo, Januari 13, 2026 jijini Dar es Salaam, wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi, Makonda amesema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha vijana kumiliki vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa kutoa maudhui yenye ubora.
Mbali na suala hilo Waziri Makonda amesema pia ana mkakati mpya wa kuanzisha timu maalum ndani ya wizara itakayoshughulika na mawasiliano ya lugha mbalimbali za Kimataifa ili kuhakikisha habari na matukio ya Serikali yanarushwa na vyombo vikubwa vya habari duniani kwa ufanisi zaidi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
