#INTERNATIONALUPDATE#INTERNATIONALUPDATE

#INTERNATIONALUPDATE
Maafisa zaidi ya 300 wa Jeshi la Polisi wa Jiji la wametangaza kuwa wanachama wa Freemason au “miungano mingine ya aina hiyo” baada ya kikosi hicho kuwataka kufanya hivyo mwezi uliopita, jaji wa Mahakama Kuu amesema.

Polisi ilitangaza mnamo mwezi Desemba kwamba uanachama wa Freemason au mashirika kama hayo yataongezwa kwenye sera yake ya vyama vinavyoweza kutangazwa.

Maafisa na wafanyakazi walitakiwa kutangaza uanachama “wa zamani au wa sasa” wa shirika au muungano wowote wa kijamii “wenye uanachama wa siri na unahitaji wanachama kusaidiana na kulindana”.

Hatua hiyo ilisababisha mashirika yenye kuwawakilisha Freemason kuanza hatua za kisheria kuhusu uamuzi wa kikosi hicho katika Mahakama Kuu yakitaka sera hiyo kusitishwa hadi uamuzi wa kesi iliyowakilishwa mahakamani utakapotolewa.

Kikosi hicho kiliongeza kwamba hakukuwa na pendekezo kwamba kimepanga kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa au wafanyakazi kwa kujitangaza hadharani kuwa wanachama wa Freemason.

Jeshi hilo lilithibitisha kwamba maafisa na wafanyakazi 316 walikuwa wametangaza uanachama wa Freemason au miungano mingine sawia na huo

#chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *