Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemkamata Denis Ogesa (28), raia wa Kenya na mkazi wa Nairobi, kwa tuhuma za kuvunja na kuiba katika tawi la Benki ya Azania lililopo mji wa Namanga, wilayani Longido.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, tukio hilo lilitokea Januari 14, 2026, saa 6:40 usiku, wakati mtuhumiwa akiwa anaendelea kutekeleza tukio hilo la kihalifu ndani ya benki hiyo ndipo alikamatwa na askari wa polisi.
Kamanda huyo amesema wakati wa kukamatwa, mtuhumiwa alikutwa na fedha taslimu jumla ya shilingi za Tanzania 91,280,000 pamoja na shilingi za Kenya 288,700, fedha zinazodhaniwa kuwa ni sehemu ya mali iliyopatikana katika tukio hilo.
Mharirir @claud_jm
#AzamTVUpdates