#HABARI: Watu wenye ulemavu wa kusikia katika Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, wameiomba Serikali kuweka wataalamu wa lugha za alama katika vituo vya afya ili kuondoa vikwazo vya mawasiliano wanapotafuta huduma za matibabu. Wakizungumza kupitia mwandishi Ferdinand Shayo, walengwa hao wameeleza kuwa kukosekana kwa wakalimani kunawafanya washindwe kuelezea changamoto zao za kiafya kwa usahihi, jambo linaloweza kupelekea kupata matibabu yasiyo sahihi.
Ombi hilo limewasilishwa mbele ya viongozi wa Serikali, ambapo wadau hao wamependekeza kuanzishwa kwa dawati maalum la matibabu litakalokuwa na wakalimani wa lugha za alama ili kurahisisha huduma. Wamesisitiza kuwa kuwepo kwa wataalamu hao kutahakikisha usiri wa mgonjwa na kumpa haki ya kupata matibabu stahiki bila kutegemea ndugu au watu baki kuingilia kati mawasiliano yao na madaktari.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.