Kiongozi mpya wa Nepal aliahidi Jumapili kufuata matakwa ya waandamanaji ya “kumaliza ufisadi” alipokuwa akianza kazi kama waziri mkuu wa mpito, baada ya maandamano ya vijana wa kizazi cha “Gen Z” kumwondoa mtangulizi wake.

“Lazima tufanye kazi kulingana na mawazo ya kizazi cha Gen Z,” alisema Sushila Karki, katika maoni yake ya kwanza kwa umma tangu alipochukua madaraka Ijumaa.

“Kile ambacho kundi hili linadai ni kumaliza ufisadi, utawala bora na usawa wa kiuchumi,” aliongeza. “Wewe na mimi lazima tuwe na nia ya kutimiza hayo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *