Mashambulizi hayo yamelenga majengo kadhaa na kusababisha mauaji ya wapalestina 13.

Kabla ya kuondoka Marekani Rubio alisema atatafuta majibu kutoka kwa maafisa wa Israel kuhusu hatua ya kuchukua katika vita vya Gaza, kufuatia shambulizi la Israel lililofanywa Qatar wiki iliyopita, likiwalenga viongozi wa Hamas, lililotia doa juhudi za usitishwaji vita.

Ziara hiyo ya siku mbili pia ina lenga kuonesha uungwaji mkono wa Marekani kwa Israel.

Umoja wa Mataifa wiki ijayo unafanya kikao maalum kuamua kuhusu kuundwa kwa dola la Palestina. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu analipinga wazo hilo vikali.

Wakati uo huo waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, ameitolea mwito dunia kuachana na undumila kuwili na kuiadhibu Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *