
Mchambuzi mmoja wa masuala ya kieneo na kimataifa wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa, si Donald Trump na si Marekani yenyewe, wote hawana uthubutu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran.
Alon Mizrahi amesema hayo katika mahojiano maalumu ikiwa ni majibu yake kwa vitisho vya hivi karibuni vya Trump vya kuishambulia tena Iran na kusisitiza kuwa, Wamarekani wanabweka tu hivi sasa hawana meno ya kung’ata mbele ya Iran.
Shirika la Habari la Fars limemnukuu Mzayuni huyo, Alon Mizrahi, akisema pia katika taarifa zake nyingine kuhusu uwezekano wa Marekani kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran, kwamba, Marekani haitofanya jambo kama hilo kwa sababu Iran ni nchi yenye nguvu kubwa.
Mchambuzi huyo maarufu wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa, Donald Trump ni mtu mdogo tu mwenye mdomo mpana ambaye anajaribu kuficha woga na udhaifu wake wa ndani ya nafsi yake kwa kutamba kwamba yeye ndiye kiongozi wa dunia, lakini madai hayo yako mbali na uhalisia wa mambo.
Kwa mujibu wa mchambuzi huyo Mzayuni, Marekani haiwezi hata kuingia vitani na kijinchi kidogo kama Honduras kwani hivi sasa Marekani inaishi katika hali ya kusikitisha, sembuse tena kuingia vitani na Iran.
Matamshi ya mchambuzi huyo wa Israel yamekuja huku vyombo vya habari vikiwa vimeripoti kabla ya hapo kwamba, washauri na washirika wa Trump, akiwemo waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, nduli Benjamin Netanyahu, wamemuonya Trump asithubutu kuanzisha vita dhidi ya Iran kwani matokeo yake hayatabiriki na kamwe Marekani haitoweza kufikia malengo yake kwenye uvamizi kama huo.
Nchi za Kiarabu za eneo hili pia kama vile Saudi Arabia, Qatar, Oman pamoja na Misri zimemuonya rasmi Trump kuhusu chokochoko zake hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.