#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko makubwa, taarifa za kifo cha Mzee Edwin Isaac Mbiliewi Mtei, kilichotokea usiku wa Januari 19, 2026, jijini Arusha.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yangu binafsi, natuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, na wote walioguswa na msiba huu,” amesema Rais Dkt. Samia.
Rais Dkt. Samia atamkumbuka Marehemu Mtei kama mmoja wa watumishi na viongozi wenye mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa kwenye eneo la fedha, mipango na uchumi, aliyehudumu katika nafasi mbalimbali ikiwemo Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (1966 – 1974), na kushiriki kuimarisha misingi ya uendeshaji wa Benki Kuu na uthabiti wa mfumo wa fedha nchini.