#HABARI: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesikitika kutangaza kifo cha muasisi wa Chama na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho, Mzee Edwin Mtei.
Mzee Mtei amefariki usiku wa kuamkia leo Januari 20, 2026 nyumbani kwake Tengeru mkoani Arusha ikiwa ni siku moja kabla Chama hakijaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo Januari 21, 1993, Mzee Mtei alikabidhiwa cheti cha usajili wa Chadema.
Chama kimeeleza kuwa, taarifa zaidi za taratibu za maombolezo, kuaga mwili na mazishi kitazitoa baadae leo.
Chama kinatangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera za chama zitapepea nusu mlingoti.
“Amepigana vita vilivyo vizuri. Mwendo ameumaliza. Imani ameilinda. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Edwin Mtei mahala pema peponi,” wameandika CHADEMA kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Instagram.