Shuhudia boti mpya ya kisasa ya Kilimanjaro IX – The Dragon of the Sea ikivinjari kwa utulivu katika fukwe zilizopo katika viunga vya Hotel Verde, Mjini Magharibi, ikivutia macho ya wageni na wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio la uzinduzi.
Safari hiyo fupi ya maonesho ilithibitisha uwezo na uimara wa boti hiyo, huku ikionesha viwango vya juu vya usalama kwa abiria.
Kilimanjaro IX yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 600 inatarajiwa kuboresha huduma za usafiri wa majini na kuongeza ufanisi wa safari kati ya Zanzibar na maeneo mengine.
#AzamTVUpdates
✍Jairo Mtitu
Mhariri | John Mbalamwezi