Serikali ya Togo imethibitisha siku ya Jumanne, Januari 20, 2026, kwamba ilimrejesha nyumbani nchini Burkina Faso rais wa zamani wa mpito Paul-Henri Sandaogo Damiba Januari 17. Damiba alipinduliwa mwaka wa 2022 na tangu wakati huo ameshutumiwa kwa kupanga majaribio kadhaa ya mapinduzi. Kurejeshwa huku kunaibua maswali kadhaa: kwa nini, vipi, na kwa maslahi gani ya kimkakati Togo ilikubali maombi ya Burkina Faso?

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Paul-Henri Sandaogo Damiba, ambaye alikuwa uhamishoni nchini Togo, alikamatwa Januari 16 na “kukabidhiwa kwa mamlaka ya Burkina Faso” siku iliyofuata, baada ya kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa ya Lomé, kulingana na taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya umma na Waziri wa Sheria.

Taarifa hiyo inabainisha kwamba Burkina Faso iliwasilisha ombi la kurejeshwa nchini humo kwa Paul-Henri Sandaogo Damiba Januari 12, hasa kwa “ubadhirifu wa fedha za umma, utajiri haramu, ufisadi, uchochezi wa kutenda makosa na uhalifu, kupokea bidhaa zilizoibwa kwa njia wizi uliyokithiri, na utakatishaji fedha.” Taarifa hiyo inabainisha kwamba utaratibu huu ulifanywa “ndani ya mfumo wa ushirikiano wa kimahakama kati ya mataifa hayo na kuheshimu utawala wa sheria.”

Kwa mujibu wa taratibu za kurejeshwa numbani kutoka nchini Togo, wizara inabainisha kwamba chumba cha uchunguzi kilikubali ombi la Ouagadougou: “Kufuatia maoni haya mazuri kutoka kwa chumba cha uchunguzi, Bw. Damiba alikabidhiwa kwa mamlaka ya Burkina Faso Januari 17, 2026,” taarifa hiyo, iliyosomwa kwenye televisheni ya umma, inaongeza.

Paul-Henri Sandaogo Damiba alichukua madaraka Januari 2022 katika mapinduzi dhidi ya rais aliyechaguliwa wakati huo, Roch Marc Christian Kaboré, kabla ya kupinduliwa miezi tisa baadaye na Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye bado yuko madarakani. Luteni Kanali Damiba alikuwa akiishi uhamishoni Lomé tangu mwezi Oktoba 2022. Alipokuwa uhamishoni Togo, alishutumiwa mara kwa mara kwa kujaribu kuvuruga utawala wa kijeshi uliomtimua madarakani.

Taarifa ya Togo inabainisha kwamba uamuzi wa Lomé ulifanywa baada ya kupokea uhakikisho kuhusu heshima ya uadilifu na utu wa Paul-Henri Damiba. Dhamana pia zilipatikana kuhakikisha kesi ya haki na kutaja “kutokuwepo kwa adhabu ya kifo.” Maneno haya yasiyoeleweka yanaacha nafasi ya shaka kuhusu ahadi gani hasa Lomé iliyopokea katika suala hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *