#HABARI: Wataalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Januari 21, 2026, wamekagua mradi na wametembelea wananchi wanufaika wa Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika kata za Mingoyo na Mnazi Mmoja mkoani Lindi kwa lengo la kukagua utekelezaji wake na kuhamasisha wananchi zaidi kujiunga katika mradi huo ambao umekamilika.
Wananchi wanaonufaika na mradi huo wameeleza kufurahishwa na faida wanazopata baada ya kufikishiwa miundombinu ya gesi asilia hadi majumbani mwao.
Bi, Mebo Mkomola, mmoja wa wanufaika, amesema matumizi ya gesi asilia yamerahisisha maisha yake na kuboresha uchumi wa familia yake, ikilinganishwa na changamoto walizokuwa wakikumbana nazo walipokuwa wakitumia kuni na mkaa.
Naye Kaimu Meneja wa Biashara ya Gesi Asilia kutoka TPDC, Mhandisi Denice Byarushengo, amesema mitambo ya kupunguza mgandamizo wa gesi iliyowekwa imesaidia kufikisha kiwango sahihi cha gesi kinachohitajika kwa matumizi ya nyumbani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)