Zaidi ya safari za ndege 2,000 zimefutwa nchini Marekani kwa sababu ya kufungwa kwa serikali
Waziri wa Usafiri Sean Duffy anaonya kuwa makato yanaweza kufika hadi asilimia 20 ikiwa kufungwa kwa serikali kutaendelea.
Waziri wa Usafiri Sean Duffy anaonya kuwa makato yanaweza kufika hadi asilimia 20 ikiwa kufungwa kwa serikali kutaendelea.
Amri za kukamatwa zinalenga maafisa 37 wa Israeli, akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kwa mashtaka ya uhalifu wa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu katika Gaza.
Rais wa Azerbaijan anasifu juhudi za ujenzi wa taifa, asante Uturuki na Pakistan kwa msaada.
Urusi yasema iko tayari kuzungumza na Marekani kuhusu Ukraine+++Rais wa Syria awasili Marekani katika ziara ya kihistoria+++Maelfu wahamishwa makwao kupisha kimbunga kingine kikubwa Ufilipino
Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimetangaza leo mchana kuwa polisi kwenye mkoa wa kaskazini wa Arusha limemkamata Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Amani…
Marekani imesema jana kuwa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeahidi kushirikiana kupunguza mvutano na kuahidi tena kuzingatia makubaliano ya amani, ambayo yameshindwa kusitisha ghasia.
Droni moja imelenga jengo la ghorofa tisa katika mji wa Dnipro mashariki mwa Ukraine mapema leo na kuwauwa watu watatu pamoja na kujeruhiwa wengine 12. Haya yameripotiwa leo na mamlaka…
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Kenya ODPP, imepongeza kukumatwa kwa mwanajeshi wa zamani wa Uingereza Robert James Purkiss, kwa tuhuma za kumuua raia wa Kenya Agnes Wanjiru zaidi…
Israel imetambua mabaki ya mateka wa hivi karibuni zaidi kurejeshwa na kundi la Hamas kutoka Gaza na kubakisha idadi ya miili mitano mingine inayopaswa kurejeshwa chini ya makubaliano ya amani…
Tayari mamia ya wananchi wamefunguliwa mashtaka kwa makosa ya jinai huku viongozi wa upinzani wakiwekwa kwenye orodha mpya ya watakaokamatwa na kushtakiwa
Maharamia hao waliiacha meli ya mfanyabiashara baada ya "kuonyeshwa nguvu", taarifa ya Jeshi la Wanamaji la Umoja wa Ulaya ilisema.
Rais wa Uturuki Erdogan ametoa wito kwa Armenia na Azerbaijan kujenga mustakabali wa amani wakati wa kusherehekea mafanikio ya Azerbaijan huko Karabakh..
Polisi ya Tanzania imesema inawasaka viongozi kadhaa wa upinzani ikiwalaumu kuhusika na maandamano ya vurugu yaliyoitikisa nchi hiyo wakati wa uchaguzi mkuu.
Wanaharakati wawili wa Kenya Bob Njagi na Nicholas Oyoo wameachiliwa huru baada ya kutoweka Uganda walikokuwa wanahudhuria mkutano wa chama cha upinzani nchini humo. Haya ni kulingana na mashirika ya…
Zaidi ya watu 200 nchini Tanzania wameshtakiwa kwa kosa la uhaini siku chache baada ya maandamano ya uchaguzi ambapo upinzani unasema mamia ya watu waliuawa. Haya ni kwa mujibu wa…
Mahakama moja ya Istanbul, Uturuki, imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na maafisa wengine 36 wa serikali yake kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu…
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO, Mark Rutte, amesema katika siku zijazo, anakusudia kuangazia zaidi uwezo wa nyuklia wa muungano huo wa ulinzi wa nchi za Magharibi, kama kingi…
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema hakuna afisa wa Marekani atahudhuria mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika Afrika Kusini, kwa madai yasiyo na ushahidi ya "kuuawa na kuchinjwa" kwa raia…
Robert James Purkiss aliyekamatwa huko Tidworth, Wiltshire mnamo 6 Novemba na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu ya Westminster siku ya Ijumaa na huenda akarejeshwa Kenya kujibu mashtaka
Trump anasema anatarajia kuandaa Mkutano wa G20 wa 2026 huko Miami.
Israel imeua karibu watu 69,000, wengi wao ni wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi ya 680,600 wengine katika mauaji ya kimbari katika Gaza tangu Oktoba 2023.
Nchini Marekani kampuni za ndege zimo kwenye ukingo wa kufuta maelfu ya safari kutokana na kufungwa kwa shughuli za serikali kuu kwa karibu siku arobaini.
Mvutano mkubwa umeibuka ndani ya vyama ndugu vya CDU na CSU baada ya kauli ya Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul kuwa hali ya Syria ni mbaya…
Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yamelaani ripoti zilizoenea za mauaji ya dhidi ya raia, baadhi majumbani mwao, katika ghasia za baada ya uchaguzi.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa Iran inatafuta amani, lakini haitashurutishwa wala kuacha mpango wake wa nyuklia. Haya yameripotiwa leo na vyombo vya habari vya serikali.
Nchi za Umoja wa Ulaya hazitatoa tena viza za kuingia zaidi ya mara moja katika mataifa ya Umoja huo kwa raia wa Urusi, kufuatia "vitendo vya hujuma na uwezekano wa…
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema leo kuwa takriban watu 100 wamerekodiwa kutekwa nyara ama kutoweka nchini Syria tangu mwanzoni mwa mwaka huku kukiwa na ripoti…
Makundi ya haki za binaadamu nchini Tanzania yamelaani ripoti za kile walichotaja "mauaji ya kulipiza kisasi" dhidi ya raia, katika ghasia za baada ya uchaguzi ambazo kulingana na upinzani, mamia…
Awali Sudan Kusini iliorodheshwa miongoni mwa mataifa ambayo yangefaidika kwa muda mnamo Oktoba 13, 2011, kulingana na mapigano nchini humo kati ya serikali ya rais Salva Kiir na makamu wake…
Uchambuzi wa data mpya kutoka kwa Ushirikiano wa Awamu Jumuishi ya Usalama wa Chakula (IPC) iligundua kuwa watoto wapatao milioni 14—mmoja kati ya watano – watakabiliwa na viwango vya njaa…
Kimbunga Kalmaegi kimesababisha upepo mkali na mvua kubwa huko Vietnam iliyopelekea watu watano kuuwawa, kuharibu majumba kung'oa mapaa ya majengo pamoja na miti.
Miongoni walioshikwa ni mfanyabiashara, Jenifer Bilikwiza Jovin almaarufu Niffer amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo Ijumaa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemuondolea vikwazo Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa anayetarajiwa kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani Jumatatu ijayo.
Hali Tanzania inaripotiwa kurudi kwenye ushuwari wake, baada ya mauaji yaliyoshuhudiwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, zilizopelekea kufungwa kwa huduma za intaneti kulikosababisha athari za…
Wanafunzi wawili Keicy Winely mwenye umri wa miaka 12 na Shanice Achieng mwenye miaka 13 kutoka Kenya, walivumbua pipa la kutupia taka linalotumia "sensor" na hufunguka bila kuguswa kwa mkono…
Mkuu wa jeshi la Ujerumani Carsten Breuer, ameonya leo kuwa Urusi haipaswi kabisa kufikiria kwamba inaweza kushinda vita dhidi ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO au hata dhidi ya mwanachama…
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anatarajia kuwa hivi karibuni, kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu kinachoratibiwa na Marekani kitawasili Ukanda wa Gaza.
Kimbunga Kalmaegi kimepiga Vietnam baada ya uharibifu mkubwa nchini Ufilipino, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua watano na kuharibu zaidi ya nyumba 2,600. Haya yamesemwa leo na maafisa nchini humo.
Miripuko imesikika leo karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, unaodhibitiwa na jeshi, siku moja baada ya wapiganaji wa RSF kusema wamekubali pendekezo la usitishaji mapigano kwa sababu za kibinaadamu.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, jana Alhamisi ilithibitisha mashtaka yote 39 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yanayodaiwa kufanywa na mbabe wa kivita wa Uganda, Joseph…
Rais wa Ujerumani Frank -Walter Steinmeier amewahimiza wafanyabiashara wa Ujerumani kufanya uwekezaji katika mradi mkubwa wa miundombinu ya reli wa Lobito kusini mwa Afrika.
Rais wa Kenya William Ruto atoa wito wa kuachiliwa kwa Wakenya wanaoshikiliwa nchini Ukraine baada ya kufanya maongezi ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Afrika imekumbwa na shinikizo kubwa la maandamano ya vijana maarufuiru Gen Z,maandamano hayo yamekuwa yakibeba ujumbe wa vijana kupinga mifumo ya kiutawala,hali ya uchumi,haki za binadamu na matumizi ya rasilimali.
Mwaka mmoja tangu kuangushwa kwa utawala wa kidikteta wa Bashar Al Assad, Syria bado imezongwa na vurugu.
Paul Biya, Rais mkongwe zaidi duniani, mwenye umri wa miaka 92 ameapishwa kuwa Rais wa Cameroon kwa muhula wa nane.
Waasi wa AFC/M23 wamewateua mamia ya mahakimu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mahakimu hao watakuwa na jukumu la kufufua…
John Okoth Ogutu, Mkenya mwenye umri wa miaka 33 aliyeishi Tanzania kwa zaidi ya miaka kumi, amethibitishwa kuuwawa kwa risasi wakati wa machafuko yaliyotokea Dar es Salaam baada ya uchaguzi.
Mchezaji Ousmane Dembele ni mshambuliaji anayeona mbele siku zote. Akikipiga na timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa (PSG). Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa.
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba Kazakhistan itajiunga na Mikataba ya Amani ya Abraham katika hatua muhimu ya kuimarisha jitihada za kutafuta amani ya Mashariki ya Kati.
Jeshi la Israeli limesema kuwa limekamilisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya kijeshi ya kundi la wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon.