Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuhukumiwa kifo kwa makosa ya uhaini tarehe 22 mwezi Agosti mwaka huu, ameikashifu hukumu hiyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kando na kuikosoa hukumu hiyo, Kabila aidha ameelani hatua ya bunge la Senate la Congo mwezi Mei kumuondolea kinga ya kutoshtakiwa, suala analosema ni kinyume na sheria na linakiuka katiba ya nchi.

Kabila pia amepinga tuhuma za ubakaji, mauaji, uhaini, uhalifu wa kivita, mauaji, utesaji wa watu pamoja na kuwaunga mkono waasi wa AFC/M23, tuhuma anazosema hazina ushahidi wowote.

Kulingana na Rais huyo wa zamani wa Congo, tuhuma zote dhidi yake zimechochewa kwa misingi ya kisiasa na wale anaosema ni viongozi ambao wanajaribu kukwepa majukumu yao.

Akizungumza Jumanne ya juma hili, Kabila amesema mashtaka yote yanayomkabili yanalenga kuunyamazisha upizani pamoja na kuwafungia wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini Congo katika ulingo wa kisiasa.

Kabila alihukumiwa kifo  na mahakama ya kijeshi bila yeye kuwepo mahakamani kwa uhaini kutokana na kile Kinshasa inamtuhumu kwa kushirikiana na waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kutatiza usalama wa Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *