
Israel imezidisha maandalizi yake ya kijeshi siku ya Jumanne kwa kuwajumuisha tena maelfu ya askari wa akiba katika safu zake ili kujiandaa na mashambulizi yaliyotangazwa kwenye mji wa Gaza baada ya karibu miaka miwili ya vita dhidi ya Hamas ya Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kundi la askari wa akiba limetoa wito kwa wenzao mjini Tel Aviv siku ya Jumanne kutoitikia wito huu kwa sababu “kitendo chochote kinacholenga kuhalalisha kuendelea kwa uhasama kwa gharama ya makubaliano ya mateka (yaliyofanyika Gaza) ni usaliti kwao na kwa raia wa Israel,” kulingana na Max Kresch, mmoja wa askari hao wa akiba.
Wengi wa askari hao wa akiba wanaachana na maisha yao, familia zao na kazi zao kwa mara ya nne au ya tano tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyoanza Oktoba 7, 2023, kwa shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la vuguvugu la Kiislamu katika ardhi ya Israel.
Jeshi la Israel linajiandaa “kwa ngazi ya kiratibu na kiutendaji kwa operesheni kubwa za kivita na uhamasishaji mkubwa wa askari wa akiba,” taarifa ya kijeshi imesema.
Katika kuidhinisha mipango ya kijeshi ya kuiteka Gaza mwishoni mwa mwezi Agosti, Waziri wa Ulinzi Israel Katz aliidhinisha uhamasishaji wa takriban askari wa akiba 60,000.
“Ndugu askari, askari wa kawaida na askari wa akiba, katika muda wote wa vita hivi, tulifanya maamuzi magumu sana (…) Lakini tuliyatekeleza kwa sababu mlitupa sisi na nchi nguvu ya kuiongoza Israel kuelekea ushindi mnono” dhidi ya Hamas, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kwenye video siku ya Jumanne.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumanne, msemaji wa jeshi la Israel kwa lugha ya Kiarabu, Avichay Adraee, amewaonya Wagaza kuhusu “kupanuka kwa operesheni za mapigano kuelekea katika Jiji la Gaza.”