
Macron ameionya Israel dhidi ya “kunyakua” au “kufanya mashambulizi dhidi ya Gaza ,” akithibitisha pamoja na Saudi Arabia uungaji mkono wake wa kutambuliwa kwa taifa la Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati wa mkutano siku ya Jumanne na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, Emmanuel Macron ameionya Israel kwamba “hakuna mashambulizi, jaribio la kunyakua, au uhamisho wa watu ambao utasimamisha kasi” yenye lengo la kuendeleza utambuzi wa taifa la Palestina.
Onyo hili linakuja wakati Paris na Riyadh zikijaribu kuhamasisha washirika wengine wa kimataifa kuhusu mpango huu, kama Ubelgiji ilivyofanya siku ya Jumatatu na Canada na Uingereza hapo awali.
Kubainisha jukumu la Ufaransa
Rais wa Ufaransa pia amekosoa uamuzi wa Marekani wa kuwanyima viza maafisa wa Palestina walioalikwa kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. “Hili halikubaliki,” amebainisha, akitoa wito kwa Washington “kubadili hatua hii na kuruhusu uwakilishi wa Palestina kwa mujibu wa makubaliano ya umoja wa Mataifa.”
Kwa kauli hizi, Emmanuel Macron anakusudia kubainisha nafasi ya Ufaransa katika mijadala ya kidiplomasia kuhusu kutambuliwa kwa taifa la Palestina, huku akilaani vikwazo vya kisiasa na kiusalama vinavyorudisha nyuma mchakato huu.