Vibali hivyo hupatikana kati ya siku moja hadi tatu, na kuondoa mfumo wa zamani wa matumizi ya karatasi, ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa na mianya ya rushwa.

‘‘Tunatumia mfumo huu katika kuhakikisha kuwa hakuna yeyote atakayetoka wala kuingia nchini bila kufanyiwa uhakika wa taarifa zao,’’ anasema Mustafa Duhulow, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji na na Uraia nchini humo.

‘‘Hadi kufikia sasa, tumetoa mafunzo kwa watu 108 kwa kutumia mfumo huu,’’ anasema Dhuhulow.

Kulingana na wataalamu, mfumo utasaidia kupambana na ugaidi, usafirishaji binadamu na uhalifu wa kuvuka mipaka.

‘‘Tutahakikisha kuwa hakuna wasafiri haramu wa kuingia wala kutoka Somalia. Tunafanya kazi kwa ukaribu na washirika wetu wa kimataifa,’’ alisema Duhulow.

‘‘Kama sehemu ya vyombo vya usalama, tutahakikisha kuwa hakuna vitisho vya Al-Qaeda, ISIS, wala Al-Shabab,’’ aliongeza.

Uwazi wa kifedha

Mfumo huu mpya utahakikisha malipo yote yanafanyika kwa uwazi bila kuwepo na mianya ya rushwa.

“Huu ni wakati mzuri sana kwa nchi yetu,” anasema Waziri wa Usalama wa Ndani wa Somalia, Abdullahi Sheikh Ismail Fartaag.

“Mfumo huu unawataka wasafiri kuweka wazi sababu za safari zao saa 24 kabla ya kusafiri.”

Utambulisho wa kimiundombinu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *