Mahakama ya Juu ya Thailand leo Jumanne imeamuru kufungwa jela mara moja kwa Waziri Mkuu wa zamani na mwanasiasa mashuhuri Thaksin Shinawatra kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Mahakama itatoa kibali (cha kuzuiliwa kwake) na afisa wa gereza la Bangkok atamchukua,” Mahakama ya Juu imeamua, kulingana na uamuzi uliosomwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Akiwa amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa ufisadi, mwanasiasa huyo mashuhuri zaidi nchini alikaa miezi sita pekee hospitalini baada ya kurejea kutoka uhamishoni mwaka wa 2023.

Mahakama ya Juu imeamua leo Jumanne kwamba hakutumikia kifungo chake cha jela ipasavyo. “Kumpeleka hospitalini haikuwa halali; mshtakiwa anajua kwamba ugonjwa wake haukuwa jambo la dharura, na kubaki hospitalini hakuwezi kuhesabiwa kama kifungo cha jela,” imesema katika uamuzi wake. Imeamuru kufungwa mara moja kwa mwanasiasa huyo wa huko Bangkok.

Takriban maafisa mia moja wa polisi wametumwa leo Jumanne asubuhi nje ya Mahakama ya Juu, ambapo wafuasi wachache wa Bw. Shinawatra wamekusanyika, wakiwa wamevalia mavazi mekundu ya chama chake cha kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *