Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameanza upya harakati za kutafuta Waziri Mkuu mpya baada ya Francois Bayrou kujiuzulu nafasi yake kufuatia kura ya kutokuwa na Imani nae iliyopigwa jana katika bunge la kitaifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Macron ambaye alitangaza kuheshimu uamuzi wa wabunge, alisema atamteua Waziri Mkuu mpya katika siku zijazo, ambaye jukumu lake la kwanza litakuwa changamoto ya kuunda bajeti itakayokubaliwa na bunge ambalo limegawanyika.

Kinyume na siku za awali, Macron anatarajiwa kuharakisha mchakato wa kumpata Waziri Mkuu mpya kutokana na hatari ya msukosuko wa kifedha na kisiasa.

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika mbele ya kumbi za miji kote Ufaransa siku ya Jumatatu usiku kusherehekea kuanguka kwa serikali ya Bayrou.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *