
Maandamano hayo yalimpelekea Waziri Mkuu aliyekuwepo Khadga Prasad Oli kujiuzulu na kuikimbia nchi.
Maandamano hayo yalisababishamauaji ya watu 51 na kuwajeruhi zaidi ya watu 1,300 wakati polisi ikijizatiti kupambana na makundi ya waandanaji waliokuwa na hasira. Maandamano hayo yalipungua tu baada ya Oli kujiuzulu.
Duru nchini humo zinasema vijana walioanzisha maandamano maarufu kama Gen Z wanamtaka Bi Karki kuchukua uongozi wa nchi.
Jaji mkuu wa kwanza na wa peke yake nchini Nepal Sushila Karki, aliye na miaka 73 ni maarufu kwa uaminifu wake, uadilifu na anayepinga ufisadi.