
Ufaransa imetambua rasmi taifa la Palestina siku ya Jumatatu, Septemba 22, 2025. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa tangazo hili wakati wa hotuba kutoka kwenye jukwaa la Mkutano Mkuu la Umoja wa Mataifa huko New York.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametambua rasmi taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu, Septemba 22, 2025. Alizungumza karibu 3:00 usiku saa za Ufaransa na Afrika ya Kati (Saa 2 usiku aAfrika Mashariki).
Takriban wilaya 86 za miji ya Ufaransa zilipeperusha bendera ya Palestina siku ya Jumatatu asubuhi licha ya upinzani wa serikali, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani. Bruno Retailleau, Waziri wa Mambo ya Ndani anayemaliza muda wake, aliwaagiza wakuu wa wilaya kusitisha maonyesho yote ya bendera, kwa kuzingatia kanuni ya kutoegemea upande wowote katika utumishi wa umma, kutoingilia sera ya kimataifa ya Ufaransa, na hatari ya “vurugu kubwa” kwa utaratibu wa umma.
Siku ya Jumapili, Septemba 21, Uingereza, Australia, Ureno na Canada zilitarajia tangazo la Ufaransa kulitambua taifa la Palestina. Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alitoa wito wa kuwepo kwa suluhu ya mataifa mawili. Hii sasa inafikisha 148, kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, idadi ya nchi zinazolitambua taifa la Palestina.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amejibu kuhusu utambuzi huu siku ya Jumapili mchana, akisema kwamba “hili halitafanyika.” “Hakuna taifa la Palestina litakaloanzishwa magharibi mwa Mto Jordan,” alibainisha.
Kwa upande wa Ufaransa kulitambua taifa la Palestina, Rais Emmanuel Macron amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya makundi ya wanasiasa na jamii ya Wayahudi.
“Kutambuliwa huku kwa taifa la Palestina kwa Ufaransa kunaambatana na hatua kama hii kutoka Andorra, Ubelgiji, Luxembourg, Ureno, Uingereza, na San Marino, ambao wamesubiri nasi kwa wakati huu,” ameongeza Emmanuel Macron.