Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hii leo kwamba kupunguzwa kwa bajeti ya misaada kumesababisha uharibifu mkubwa. Guterres ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutoa taswira mbaya ya utaratibu wa dunia. Guterres ameongeza kuwa, hatua hiyo imekuwa kama adhabu ya kifo kwa watu wengi bila ya kutaja Marekani ambayo ndio mhusika mkubwa wa kupunguzwa misaada.

Katika hotuba iliyojaa hali ya kutisha, Guterres ameashiria kuwepo kwa hali mbaya ya migogoro katika idadi inayoongezeka ya nchi na kuonya juu ya hatari ya kuenea kwa silaha za nyuklia. Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anasema migogoro mingi inaendelea bila kudhibitiwa, hali ya watu kufanya makosa bila kuadhibiwa, na sheria kutoheshimiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *