Wapiga kura nchini Guinea wameunga mkono kwa kishindo kura ya maoni ya katiba mpya ambayo inaweza kuruhusu kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya kuwania urais ikiwa ataamua. Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa wapiga kura wameunga mkono Katiba mpya kwa asilimia 90.6na asilimia 9.4 ndio wamekataa mabadiliko hayo. Matokeo hayo ni kwa kuzingatia asilimia 91 ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa kura ya maoni. Idadi ya jumla ya waliojitokeza kupiga kura haijatolewa, lakini maafisa walikuwa wamehesabu zaidi ya kura milioni 4.8 kati ya zaidi ya wapiga kura milioni 6.6 waliojiandikisha, kumaanisha kuwa waliojitokeza walikuwa wamezidi asilimia 70. Doumbouya alinyakua mamlaka nchini Guinea mwaka 2021. Unyakuzi huo ulikuwa ni sehemu ya wimbi la mapinduzi nane ambayo yaliindama kanda ya Afrika Magharibi na Kati, kati ya mwaka 2020 na 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *