Siku mbili baada ya ndege zisizo na rubani kuonekana juu ya anga ya uwanja wa ndege wa Copenhagen, ndege hizo zimeonekana usiku wa umatano kuamkia Alhamisi kwenye viwanja vinne vya ndege vya Denmark. Uwanja wa ndege wa Aalborg, ambao pia unatumika kama kituo cha kijeshi, ulifungwa kwa saa kadhaa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ndege zisizo na rubani ambazo asili yake hazijulikani zilmeonekana usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, Septemba 25, kwenye viwanja vinne vya ndege vya Denmark, na kusababisha mojawapo ya viwanja hivyo kufungwa kwa saa kadhaa, polisi imesema.

Ndege hizo zisizo na rubani zimeonekana kwenye uwanja wa ndege wa Aalborg (kaskazini), uwanja wa ndege wa Esbjerg (magharibi), na uwanja wa ndege wa Sonderborg (kusini), pamoja na kituo cha kambi ya jeshi la wanaanga cha Skrydstrup (kusini), kabla ya kuondoka eneo hilo. Siku ya Jumatatu, ndege zisizo na rubani ambazo asili yake hazijulikani zilikuwa tayari zimeruka juu ya uwanja wa ndege wa Copenhagen na uwanja wa ndege wa Oslo katika nchi jirani ya Norway, na kuzuia usafiri kwa saa kadhaa.

Ndege hizo zisizo na rubani zimeonekana karibu na viwanja vya ndege vya Aalborg (kaskazini), Esbjerg (magharibi), na Sonderborg (kusini), na kituo cha anga cha Skrydstrup (kusini), kabla ya kuondoka eneo hilo.

Kituo cha Aalborg kilifungwa kwa saa kadhaa kabla ya kufunguliwa tena. “Haikuwezekana kuangusha ndege zisizo na rubani, ambazo ziliruka juu ya eneo kubwa sana. […] Pia hatukukamata waendeshaji” wa ndege hizi zisizo na rubani, amesema Jesper Bojgaard Madsen wa Polisi ya Jimbo la Jutland Kaskazini, kuhusiana na matukio ya Aalborg.

Tukio hili pia limeathiri jeshi la Denmark, polisi imesema, kwani eneo hilo pia linatumika kama kituo cha kijeshi. Jeshi limebainisha kwamba lilikuwa likisaidiana na polisi katika uchunguzi wao, bila kutoa maelezo zaidi.

Vikosi vya usalama vya Jutland Kusini, ambavyo vimeripoti juu ya maeneo mengine yaliyolengwa, vimebaini kwamba ndege zisizo na rubani ziliruka “zikiwa na taa zao na zilitazamwa kutoka ardhini,” ingawa haikujulikana ni aina gani ya ndege au sababu ya kuruka kwa ndege hizo kwenye viwanja hivyo vya ndege.

Polisi wamesema wanachunguza kwa ushirikiano na idara ya ujasusi ya Denmark, PET, na jeshi.

Urusi katika uangalizi

Siku ya Jumatatu, ndege zisizo na rubani ambazo hazijatambuliwa tayari zilikuwa zimeruka juu ya uwanja wa ndege wa Copenhagen na uwanja wa ndege wa Oslo katika nchi jirani ya Norway, na kuzuia usafiri wa ndege kwa saa kadhaa. Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alishutumu “shambulio kubwa zaidi kwenye miundombinu muhimu,” akisema “inawezekana” kwamba Urusi imehusika. Moscow imesisitiza kuwa haikuhusika.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Septemba, nchi kadhaa za NATO za Ulaya zimeshutumu uvamizi katika anga zao, zikiilaumu Urusi, ambayo imekana kuhusika.

Mwishoni mwa juma lililopita, viwanja vya ndege vya Ulaya, vikiwemo vile vya Brussels, London Heathrow, Berlin, na Dublin, pia vilitatizwa na mashambulizi ya mtandaoni ambayo asili yake haijafichuliwa.

Na AFP na Reuters

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *