Miaka 20 iliyopita, alikuwa katika jela ya Marekani nchini Iraq kwa ajili ya uanachama wake katika kundi la Islamic State. Siku ya Jumatano, Septemba 24, almezungumza katika Umoja wa Mataifa mjini New York kama rais wa mpito wa Syria. Ahmed Al-sharaa ametoa wito wa kukomeshwa kwa mashambulizi ya Israel katika nchi yake, ambayo, amesema, yanatishia kusababisha “migogoro na mapambano mapya katika ardhi yetu.”

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mara ya mwisho kwa rais wa Syria kuhutubia Umoja wa Mataifa ilikuwa miaka 58 iliyopita, mwaka 1967. Kwa hiyo taswira ya Ahmed Al-sharaa akiwahutubia wawakilishi wa dunia ilikuwa yenye nguvu. Hata zaidi ikizingatiwa kwamba chini ya mwaka mmoja uliopita, alikuwa tu kiongozi wa kundi la waasi lililotangazwa na nchi nyingi kuwa la kigaidi, na Syria ilikuwa chini ya vikwazo vya kimataifa.

“Sera za Israel zinakinzana na msimamo wa kimataifa wa kuunga mkono Syria,” ametangaza kiongozi huyo wa zamani wa wanajihadi, ambaye aliingia madarakani baada ya kuangushwa kwa rais wa zamani Bashar  Al Assad mnamo mwezi Desemba 2024. “Ili kukabiliana na hili, Syria inasalia kujitolea kufanya mazungumzo (…) na tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusimama upande wetu katika kukabiliana na mashambulizi haya.” Syria ndiyo inayolengwa na mashambulizi na uvamizi wa mara kwa mara na Israel, ambayo inatumia fursa ya wakati wa udhaifu kwa adui huyu wa kihistoria.

Kujadili makubaliano ya usalama na Israel

Moja ya malengo ya ziara ya Ahmed Al sharaa ni mazungumzo ya makubaliano ya usalama na Israel. Makubaliano haya yanasukumwa na Marekani, ambayo ina matumaini kuhusu uwezekano wake, lakini Ahmed Al-sharaa anaishutumu Israel kwa kuchelewesha mazungumzo.

Akirejelea mivutano ya kidini inayoendelea kuisambaratisha nchi yake, ameahidi “kupambana na udini” na “kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika katika umwagaji damu.” “Tumeunda tume ili kubaini ukweli na kutoa fursa kwa misheni za kutafuta ukweli za Umoja wa Mataifa,” amebainisha.

Mikutano na viongozi wa kimataifa

Baada ya kuwasili New York siku chache zilizopita, rais wa mpito wa Syria amefanya mikutano mingi, haswa na Amir wa Qatar, Rais wa Ufaransa, na Waziri Mkuu wa Italia, kila wakati akionekana akitabasamu pamoja na viongozi wengine. Onyesho moja hasa linatoa muhtasari wa maendeleo yaliyopatikana: Ahmed Al-sharaa alishiriki katika mkutano ambao alihojiwa na Jenerali mstaafu David Petraeus, kamanda wa zamani wa majeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati wakati rais wa sasa, wakati huo mpiganaji wa kijihadi, alipozuiliwa nchini Iraq na Marekani.

Waziri wake wa Mambo ya Nje, Assaad al-Shaibani, aliwasili Washington wiki iliyopita kwa ziara ya kiserikali. Kulingana na wizara hiyo, alikutana na maseneta wa Marekani na wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje. Pia alikutana na Tume ya Marekani kuhusu uhuru wa kidini wa kimataifa, wakati ambapo jumuiya ya kimataifa inashinikiza mamlaka mpya ya Syria kuwalinda wachache katika nchi hii yenye dini nyingi, iliyotikiswa katika miezi ya hivi karibuni na ghasia za kijamii.

Tangu aingie madarakani, Ahmed Al-sharaa amebadilisha vazi lale kama mpiganaji na kuwa mkuu wa nchi, akikutana na viongozi wa kigeni, akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei nchini Saudi Arabia. Trump alitangaza kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Damascus.

Wasyria Waandamana kumuunga mkono na kumpinga Ahmed AlS sharaa

Akiwa rais wa kwanza wa Syria kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka 58, ziara ya Ahmed Al-sharaa ilizusha maandamano mjini New York. Akiwa ameshikilia bendera za Syria, saa kadhaa kabla ya hotuba yake, Wasyria zaidi ya mia moja walimsubiri Ahmed Al sharaa karibu na jumba la Umoja wa Mataifa.

“Niko hapa kwa sababu hatimaye tuna sababu ya kuwa hapa baada ya zaidi ya miaka 50. Ni chanzo cha fahari na furaha hatimaye kuwa hapa, pamoja na watu wetu na kuwaona wakiwa wameungana,” amesema mmoja wa waandamanji hao.

Katika eneo hilo, hata hivyo, Wasyria wengine pia wameandamana… lakini dhidi ya kiongozi huyo wa muda. “Kiongozi wa magaidi duniani yuko hapa Umoja wa Mataifa. Kiongozi huyu na watu wanaomuunga mkono wamefanya mauaji mengi, mauaji ya halaiki na mauaji ya kikabila dhidi ya walio wachache. Sasa anatawala Syria!”

Wakimbizi milioni moja wa Syria wamerejea kutoka nje ya nchi tangu kuanguka kwa utawala wa rais wa zamani Bashar Al Assad mwezi Disemba, Umoja wa Mataifa umetangaza siku ya Jumatano. Umoja wa Mataifa pia umetaka msaada zaidi ili kuwawezesha Wasyria wengine kufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *