Mikutano ya hadhara imepangwa katika miji mikubwa ya Madagascar leo Alhamisi hii, Septemba 25, kupinga kukatwa kwa umeme na maji, hali ambayo imekuwa mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni, na kudumaza maisha ya kila siku ya wakaazi na kuchochea hali ya kutoridhika ilnayozidi kuenea. Kwa madai ya kutaka kuepuka fujo za umma huko Antananarivo, mamlaka imepiga marufuku mikusanyiko yote na kutaka vikosi vya usalama kuwa imara kwa siku hii, ambayo inaonekana kama kipimo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kamwe katika historia ya nchi hiyo hakuna mitandao ya kijamii inayotumiwa kwa kutoa wito wa maandamano ya amani huko Antananarivo. Katika wiki iliyopita, wito za maandamano zimekuwa zkiongezeka kwenye mitandao ya kijamii. Mashirika ya kiraia, wasanii, watumiaji wa mitandao, na wawakilishi wa upinzani wanaongeza wito wao wa maandamano ya amani kupinga ukosefu wa maji na umeme.

Nembo ya manga “One Piece”, ambayo tayari inatumiwa na waandamanaji nchini Nepal, na wakati huu ikirejelewa kwa watu mbalimbali nchini Madagascar, imekuwa ikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook wiki hii. Ishara ya kujiunga katika maandamano, wale wanaorusha nembo hiyo kwenye mitandao ya kijamii pia wanaelezea hasira zao kwa ahadi tupu za kisiasa, ufisadi ulioenea, na upendeleo.

Wengine bado wanashtumu maisha ya anasa ya watoto wa wanasiasa wanaojivunia utajiri wao kwenye mitandao ya kijamii. Maisha ya kila siku mbali na yale yanayopatikana kwa watu milioni 29 kati ya milioni 30 wa Madagascar.

Lakini baadhi ya kurasa pia zimekuwa zikisambaza kwa wingi jumbe ambazo zinatia wasiwasi mamlaka: anwani za maafisa wa serikali wanaotakiwa kulengwa au mfumo unaotumiwa kwa kutengeneza peke yako mabomu ya kienyeji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *