
Nchini Cameroon, siku tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa urais wa Oktoba 12, serikali imeonya wanasiasa, hasa wagombea katika uchaguzi huu, siku ya Jumatano, Septemba 24, dhidi ya usumbufu wowote unaoweza kutokea kwa utulivu wa umma. “Hakuna machafuko kabla, wakati, au baada ya siku ya uchaguzi yatavumiliwa,” ameonya Paul Atanga Nji, akihutubia maafisa wa serikali na vikosi vya ulinzi na usalama.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Yaoundé, Polycarpe Essomba
Nchini Cameroon, wagombea wamepewa onyo. “Kuna wagombea ambao wana malengo mengine kwa kujificha numa ya uchaguzi huu wa urais kupinga mamlaka ya serikali, kuhubiri ghasia, na kuhimiza machafuko ya kijamii ambayo yatavuruga utendakazi mzuri wa taasisi za jamhuri.” “Watu hawa watakinzana na utawala kwa sababu sheria itatawala na hakuna utovu wa nidhamu utakaovumiliwa,” ametangaza Paul Atanga Nji.
Kuhusu mijadala inayoendelea ndani ya safu ya upinzani, ambayo inalenga kuteuliwa kwa mgombea wa maridhiano kutoka kwa wagombea kumi na mmoja wanaompinga Rais Paul Biya, waziri amekuwa muwazi. Mgombea huyu, ikiwa atateuliwa, hatakuwa na athari kwa mpangilio halisi wa kura.
“ELECAM haitambui mipango hii”
Kwa utawala na ELECAM, bado kutakuwa na wagombea kumi na wawili tu. “Kuna wagombea kumi na wawili ambao watashiriki katika uchaguzi wa urais. Kwa hiyo kutakuwa na kadi za kupigia kura kumi na mbili katika kila kituo cha kupigia kura zinazowakilisha wagombea kumi na wawili. Nasikia miungano isiyo ya asili, wakati mwingine mgombea wa maridhiano, wakati mwingine mgombea mmoja. ELECAM haitambui mipangilio hii.” “Wale walionuia kujiondoa walipaswa kufanya hivyo kabla ya kura kuchapishwa,” amebainisha.
Paul Atanga Nji alihitimisha hotuba yake kwa kukaribisha hali ya utulivu iliyopo katika eneo la pwani, akitoa wito kwa wanajeshi, polisi, na maafisa wote wa utawala katika eneo hilo kuwa macho kwa sababu “adui halali kamwe,” ametangaza.