
Hayo yameelezwa leo na Harsh Vardhan Shringla ambaye ni mbunge wa eneo hilo la Darjeeling aliyesema kuwa vifo hivyo vilitokana pia na kimbunga cha Jumamosi usiku. Kiongozi huyo ameendelea kuwa mbali na vifo, maeneo yaliyo kando na milima yameathirika pakubwa huku barabara zikiwa zimeharibiwa.
Katika nchi jirani ya Nepal, mvua kubwa imesababisha pia maporomoko ya udongo na kusababisha vifo vya karibu watu 47 huku 35 kati ya hao wakiripotiwa kufariki katika katika wilaya ya Ilam-mashariki inayopakana na India.