Jeshi la polisi nchini Tanzania katika taarifa limesema limeanzisha uchunguzi kufuatia ripoti kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa  wanafamilia wa Humphrey Polepole- aliyekuwa balozi wa taifa hilo la Afrika Mashariki nchini Cuba kwamba ametekwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Aidha kulingana na taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi katika taifa hilo la Afrika Mashariki, bado wa linaendelea kumsubiri Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai baada yake kutumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria za Tanzania kuripoti katika Ofisi zake kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali anazodaiwa kutoa kupitia mitandao ya kijamii.

Awali  familia ya Humphrey Polepole ilikuwa imethibitisha kuwa mpendwa wao alitekwa na watu wasiojulikana wakati akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumatatu ya wiki hii.

Kulingana na familia yake, tayari wametoa taarifa kwa idara ya polisi kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mpendwa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *