
Eswatini imepokea wahamishwaji wengine 10 kutoka Marekani chini ya mpango wa Washington wa kuhamisha wahamiaji kwenda nchi za ulimwengu wa tatu, kulingana na taarifa leo Jumatatu Oktoba6, 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mamlaka ya magereza nchini humo imetangaza kuwasili kwa watu 10 na kuwekwa kizuizini, bila kutaja utambulisho wao wala uraia wao. Kundi la kwanza la wahamiaji watano lilitumwa kutoka Marekani kwenda Eswatini katikati ya mwezi wa Julai. Mmoja wao alirejea nchini kwao, Jamaica.
Rais Donald Trump, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili na kuapishwa mnamo Januari 20, 2025, analenga kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji haramu kutoka nchini Marekani. Utawala wake unajaribu kuzidisha kuwafukuza na kuwatuma katika nchi za ulimwengu wa tatu kama sehemu ya sera hii ngumu.
Wahamiaji watano wa kwanza waliofukuzwa nchini Eswatini mwaka huu walitoka Vietnam, Jamaica, Laos, Cuba, na Yemen. Mmoja wao, mwenye asili ya Jamaika, tayari amerejeshwa nyumbani kutokana na ushirikiano wa serikali yake.
Wengine wawili wanatarajiwa kurejeshwa makwao hivi karibuni, kulingana na taarifa ya Eswatini.
Eswatini, taifa dogo lenye utawala wa kifalme lenye milimani mingi linalopakana na Afrika Kusini, halijafichua masharti ya makubaliano yake na utawala wa Trump na linakabiliwa na hatua za kisheria kutoka kwa wanaharakati wa ndani ambao wanaona mpango huo ni kinyume cha sheria.
Wanaharakati wa haki za binadamu na wanasheria pia wamepinga mazingira wanaofanyiwa watu walioffukzwa nchini Marekani, huku kundi la kwanza likizuiliwa katika kifungo cha upweke.
© Reuters 2025