Mgombea ubunge wa Jimbo la Mkinga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Twaha Mwakioja, ameahidi kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 35 endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwaongoza baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mwakioja alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Sigaya, wilayani Mkinga, mkoani Tanga, akibainisha kuwa mradi huo utakuwa suluhisho la kudumu kwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa jimbo hilo.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates