Wakati mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza yameingia mwaka wake wa pili, hivi karibuniRais Donald Trump wa Marekani aliwasilisha mpango wenye vipengele 20 akidai usitishaji vita huko Gaza.
Mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wenye vipengele 20 wa kumaliza vita huko Gaza umeafikiwa kwa masharti Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS. Kusitishwa kwa mapigano na kubadilishana wafungwa, kuondolewa kwa Israel kutoka Gaza, ujenzi mpya wa Gaza, kuundwa kwa serikali ya mpito, na kuwapokonya silaha Hamas ni miongoni mwa vipengele muhimu vya mpango wa Trump kuhusu Gaza. Baada ya Hamas kutoa jibu chanya japo kwa masharti kwa mpango huo kumeibuka mvutano katika baraza la mawaziri la utawala wa kizayuni wa Israel.
Kati halia ambayo Netanyahu tayari amekubaliana na mpango wa Trump, kumeibuka mzozo mkubwa ndani baraza lake la mawaziri kuhusiana na suala hili. Mizozo hii inajikita katika mihimili kadhaa.
Mhimili wa kwanza ni kwamba, baadhi ya wajumbe wa baraza la mawaziri, akiwemo Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich, mawaziri wa usalama wa ndani na fedha, ni wapinzani wakubwa wa mpango huo na wanaamini kwamba vita vya Gaza vinapaswa kuendelea. Kwa maneno mengine ni kuwa, mawaziri hao wanaendelea kusisitiza juu ya pendekezo la uwongo kwamba inawezekana kuwakomboa wafungwa wa Kizayuni kwa njia ya vita na kwamba hakuna haja ya kuwepo makubaliano ya kisiasa na Hamas. Wanaona makubaliano haya kama mafanikio ya kisiasa kwa Hamas.

Mhimili mwingine wa mvutano ndani ya baraza la mawaziri la Netanyahu ni kuondoa kijeshi Israel kutoka Ukanda wa Gaza. Kuondoka kijeshi Israel kutoka Gaza kumekabiliwa na upinzani kutoka kwa mawaziri wa mrengo wa kulia katika baraza la mawaziri la Netanyahu, ambao wanataka kuendeleza vita hadi Hamas iangamizwe kabisa. Kwa upande mwingine, baadhi ya wajumbe wa baraza la mawaziri la Netanyahu wanaamini kuwa kujiondoa Gaza kunakinzana na mpango wa kukalia kimabavu kikamilifu ukanda huo.
Kwa muktadha huo, wanapinga sio tu kujiondoa kutoka Gaza bali pia mpango wa kuunda serikali ya mpito katika ukanda huo, kwa sababu Hamas, kwa kujibu mpango huo wa Trump, ilitangaza kuwa taifa huru la Palestina linapaswa kuundwa huko Gaza. Kwa hakika, ijapokuwa Hamas haijapinga kwa uwazi usimamizi wa kimataifa wa utawala wa Gaza, imesisitiza haja ya kuundwa taifa huru la Palestina.
Tofauti hizi za kimitazamo katika baraza la mawaziri la Netanyahu zimefichuliwa hata katika kauli za maafisa wao. Msemaji wa baraza la mawaziri la Israel alisema katika taarifa yake kwamba, hakuna kitu kinachoitwa kusitishwa vita huko Gaza, na kwamba ni kusimamishwa kwa muda kwa mashambulizi na mashambulio ya mabomu.

Wakati huo huo, kura ya maoni ya Ma’ariv inaonyesha asilimia 53 ya Waisraeli na asilimia 41 ya wapiga kura wanaunga mkono muungano unaotawala, lakini mawaziri wa mrengo wa kulia wametishia kuiangusha serikali. “Hatutakuwa sehemu ya kushindwa kitaifa ambapo hilo litakuwa doa la fedheha ya milele na kuwa bomu la saa la mauaji yajayo,” amesema Itamar Ben-Gvir.
Kwa kuzingatia tofauti hizi za kimtazamo ndani ya baraza la mawaziri la Israel, inaingia akilini nukta hii kwamba Trump au Netanyahu, au wote wawili, wanajaribu kutumia vyema jibu la Hamas la kuwaachilia mateka wote wa Israel na kujinufaisha nalo. Kwa hiyo, licha ya upinzani usio wa moja kwa moja wa Hamas, Rais wa Marekani ameonyesha kujizuia na matakwa yake mengine kwa wakati huu na akakubali majibu.
Hata hivyo utawala ghasibu wa Israel unaodai kusitisha mashambulizi dhidi ya Gaza umewaua shahidi Wapalestina wengine 65 katika muda wa saa 24 zilizopita na hivyo kuacha mafanikio ya mpango wa Trump ya kuanzisha usitishaji vita huko Gaza katika hali tata na isiyofahamika.