
Katika kujibu ujumbe wa Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu mazungumzo ya Iran na Marekani, Wizara ya Ulinzi na Msaada Kwa Jeshi la Iran imesisitiza katika taarifa kwamba: Siri ya mafanikio endelevu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufuata kamilifu na bila kusitasita amri na hatua za Amiri Jeshi Mkuu.
Taarifa hiyo imesema Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu siku zote alikuwa akisisitiza kwamba ushindi wa mwisho ni wa Uislamu na kwamba, safu ya makafiri pamoja na ukubwa wake wote, fahari, anasa na makombora yote unayorusha lakini hatimaye italazimika kurudi nyuma mbele ya umma na mhimili wa Kiislamu.
Imesema kwa msukumo na moyo aali wa kiongozi huyo shupavu, mazingira ya sasa ni dhihirisho la kushindwa maadui mbele ya vita vya hamasa, ustahimilivu, utambuzi na uaminifu wa taifa tukufu linalolea mashahidi la Iran ya Kiislamu.
Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema, ujumbe wa hivi karibuni wa wazi, wenye busara, unaozingatia ukweli wa mambo, na unaotatua matatizo yaliyopo, wa Kiongozi Muadhamu na Amiri Jeshi Mkuu kuhusu Mkataba wa Maelewano wa Islamabad unaonyesha kwamba tukio hili sio mwisho wa njia, bali ni mwanzo wa njia yenye masharti kwa ajili ya kupigania haki za taifa la Iran mkabala wa maadui watenda jinai na wasioaminika.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa ujumbe muhimu wa Kiongozi mpendwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni chanzo cha matumaini kwa taifa la Iran na onyo kwa maadui waliokata tamaa. Imesema, mbali na kusisitiza dhamira ya uaminifu kwa viongozi wa nchi, taarifa hiyo pia inaashiria ulazima wa kudumishwa mshikamano na umoja wa kitaifa chini.
Wizara ya Ulinzi ya Iran sambamba na kuthamini ujumbe wa kistratijia wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, imetangaza, sambamba na vyombo vingine vya kijeshi na vya dola, utayari wake kamili wa kusaidia na kutekeleza amri za wazi za Amiri Jeshi Mkuu kwa ajili ya kulinda haki za watu wa Iran.