Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imekamilisha ziara ya kukagua maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Afisi za Uchaguzi za wilaya saba za Unguja.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Tume Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jaji George Kazi amesema lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha maandalizi yote yanafanyika kwa wakati na kila kitu kinakwenda vizuri.
“Tume inataka kuhakikisha kila Afisi ya wilaya ipo tayari katika kuendesha Uchaguzi na imepokea vifaa vya kutosha kuelekea katika uchaguzi” amesema Mwenyekiti huyo.
Katika hatua nyingine Jaji Kazi ameongeza kuwa ziara kama hiyo itafanyika kisiwani Pemba ambapo wilaya nne zitatembelewa ili kukagua utayari wa maandalizi kuelekea katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Tume hiyo ameeleza kuwa kwasasa Tume inasubiri siku kwaajili ya kutawanya vifaa hivyo katika vituo vya kupiga kura.
Imeandaliwa na @moseskwindi