Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, iliyopo katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga, umeanzisha kampeni endelevu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mienendo ya kiikolojia ya tembo.

Mpango huo ni miongoni mwa hatua za kudhibiti uvamizi wa wanyama pori, hususan tembo, katika makazi ya watu na mashamba yanayopakana na hifadhi hiyo, ikiwa ni juhudi za kuimarisha uhusiano mzuri kati ya binadamu na wanyama pori.

Imeandaliwa na Jairo Mtitu
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *