Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yamehodhi maeneo kwa muda mrefu bila kuyaendeleza, yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa.
Amesema makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kueleza hatma ya maeneo hayo, vinginevyo serikali itayarejesha kwa wananchi ili yatumiwe kwa maendeleo mengine ya kiuchumi.
Waziri Mkuu amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti ubadhirifu wa rasilimali ardhi na kuhakikisha maeneo ya madini yanachangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates