
Katika kuadhimisha mwaka wa pili wa Vita vya Gaza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza wito wake wa usitishaji wa kudumu wa vita Gaza, akielezea maafa ya vita hivyo kama maafa ya kibinadamu yasiyokuubalika.
Antonio Guterres aliadhimisha kumbukumbu hiyo kwa kusihi kukomeshwa kwa ghasia, huku pia akiidhinisha mpango wa Marekani kama njia inayowezekana ya “amani”.
Guterres alirudia wito wake “kwa uharaka zaidi” wa kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa huru bila masharti kwa wafungwa.
Alielezea hali hiyo kama “janga la kibinadamu kwa kiwango ambacho kinapingana na ufahamu.”
Alitoa wito kwa pande zote “kuacha kuwafanya raia kulipa kwa maisha yao na mustakabali wao.”
Vita hivyo, vilivyoanza miaka miwili iliyopita, vimesababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 67,000, kujeruhiwa karibu wengine 170,000, maelfu ya watu kupotea, kuwa wakikimbizi zaidi ya watu milioni mbili, na kusababisha uharibifu mkubwa katika Ukanda wa Gaza.
Jumanne ya jana Oktoba 7 ilisadifiana na kutimia miaka miwili tangu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilipotekeleza operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa na kutoa pigo kubwa na la kihistoria dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Operesheni ya kimbunga cha al-Aqsa ilifanyika katika eneo la mpaka kati ya Ghaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel. Operesheni hiyo ilianza wakati wa alfajiri. Vikosi vya Hamas kwanza walipiga maeneo ya Wazayuni kwa kutumia maroketi na walirusha makombora 5,000. Baada ya hapo, walivuka ukuta uliojengwa na jeshi la Israel na kuingia kwenye maeneo ya walowezi wa Kizayuni. Zaidi ya wanajeshi 1,400 wa Israel waliangamizwa na 3,500 wengine walijeruhiwa kwenye operesheni hiyo ya kishujaa.