
Von der Leyen ameyasema haya katika hotuba yake huko Strasbourg, kufuatia majaribio kadhaa ya Urusi kukiuka usalama wa anga ya Ulaya.
“Msifanye kosa lolote, hii ni sehemu ya mtindo unaozidi kutia wasiwasi. Katika umoja wetu, nyaya za chini ya bahari zimekatwa, huduma katika viwanja vya ndege zimetatizwa na chaguzi zimelengwa na ushawishi wakati wa kampeni. Haya si mambo ya ghafla tu, ni kampeni inayoendelea ya kuwatia wasiwasi raia wetu, ya kutupima, kuugawa umoja wetu na kuumaliza nguvu uungaji mkono wetu kwa Ukraine. Hivi ni vita vya mbinu tofauti na tunastahili kuvichukulia kwa umuhimu mkubwa,” alisema Von der Leyen.
Von der Leyen amesema katika siku za hivi karibuni,atawasilisha mpango wa jinsi ya kuimarisha uwezo wa Umoja wa Ulaya katika maeneo tisa muhimu ikiwemo usalama wa anga, silaha na vita vya kimtandao kufikia mwaka 2030.