Makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza yameanza kutekelezwa saa sita mchana kwa saa za mashariki ya kati, jeshi la Israel limetangaza leo Ijumaa, Oktoba 10, baada ya serikali ya Israel kuidhinisha makubaliano yaliyofikiwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas. Zoezi linalofuata ni kuachiliwa kwa mateka ndani ya saa 72, pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel limetangaza kwamba usitishaji vita huko Gaza umeanza kutekelezwa tangu saa sita mchana saa za Mashariki ya Kati. Mapema asubuhi, shirika la Ulinzi wa Raia wa Gaza lilitangaza kuwa vikosi vya Israel vimeondoka katika maeneo kadhaa ya Mji wa Gaza na maeneo mengine ya kusini mwa ardhi hiyo.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump, yanatoa fursa ya kurejeshwa mateka 48 wa Israel wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza, ambao angalau 28 kati yao walifariki, kulingana na serikali ya Israel. Idadi hii ni pamoja na mwanajeshi aliyeuawa mwaka 2014 ambaye mabaki yake yanaaminika bado yanashikiliwa na Hamas.

Israel imechapisha orodha ya wafungwa 250 wanaostahili kuachiliwa kwa kubadilishana na mateka

Watu wakikumbatiana chini ya bango linaloonyesha picha za mateka baada ya tangazo kwamba Israel na Hamas wamekubaliana juu ya awamu ya kwanza ya usitishaji vita huko Gaza mnamo Oktoba 9, 2025.
Watu wakikumbatiana chini ya bango linaloonyesha picha za mateka baada ya tangazo kwamba Israel na Hamas wamekubaliana juu ya awamu ya kwanza ya usitishaji vita huko Gaza mnamo Oktoba 9, 2025. REUTERS – Ronen Zvulun

Israel imechapisha orodha ya “wafungwa 250” kwa sababu za usalama wanaostahili kuachiliwa kwa kubadilishana na mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, ambao wataachiliwa kama sehemu ya usitishaji vita na Hamas.

Orodha ya wafungwa, iliyochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Sheria ya Israel, haijumuishi wafungwa wakuu wanaoashiria mapambano ya silaha ya Palestina dhidi ya Israel, ambao majina yao Hamas ilikabidhi kwa wapatanishi kwa matumaini ya kuachiliwa kwao, kama vile Marwan Barghouthi, Ahmad Saadat, Hassan Salameh, au Abbas Al-Sayyed wanaotumikia kifungo cha maisha huko Israel.

Benjamin Netanyahu anatumai Israel inaweza kusherehekea “siku ya furaha ya kitaifa” mapema Jumatatu jioni

Waziri Mkuu wa Israel ameelezea matumaini yake leo Ijumaa kwamba nchi yake inaweza kusherehekea “siku ya furaha ya kitaifa” mapema Jumatatu jioni kwa kurejea kwa mateka wote ambao bado wanazuiliwa katika Ukanda wa Gaza. “Miaka miwili iliyopita, sikukuu ya Simhat Torah ikawa siku ya maombolezo ya kitaifa. Mwaka huu, kwa msaada wa Mungu, Simhat Torah itakuwa siku ya furaha ya kitaifa, furaha kwa kurudi kwa ndugu na dada zetu wote mateka,” Benjamin Netanyahu amesema katika hotuba yake kwa taifa. Mwaka huu, Simchat Torah inaanza Jumatatu jioni.

Pia amesema kuwa kati ya mateka 48 (47 waliotekwa nyara Oktoba 7, 2023, na mwanajeshi aliyeuawa mwaka 2014 ambaye mabaki yake yapo mikononi mwa Hamas), 20 wako hai na 28 walifariki, hivyo kuonekana kuthibitisha kwa mara ya kwanza vifo vya mateka wawili (mwanafunzi wa Nepal na askari wa Israel) ambapo Israel haijatangaza kifo chake hapo awali).

Qatar inataja “jukumu la pamoja” kwa mafanikio ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya Gaza

Waziri Mkuu wa Qatar, mpatanishi mkuu katika vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas, amesema leo Ijumaa kwamba mafanikio ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza ni “jukumu la pamoja.” “Mafanikio ya awamu hii ni jukumu la pamoja la kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano hayo na kuleta amani na utulivu,” Waziri Mkuu Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amesema katika taarifa iliyotolewa Ijumaa.

Maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza yanasalia “hatari sana” kwa wakazi, jeshi la Israel linaonya

Katika Ukanda wa kaskazini wa Gaza, “ni hatari sana kukaribia maeneo ya Beit Hanoun, Beit Lahia, Shujaiya [kitongoji cha mji wa Gaza] na maeneo mengine ambako majeshi ya Israel yamepiga kambi,” imesema taarifa kutoka kwa Kanali Avichay Adraee, msemaji wa jeshi la Israel anayezungumza Kiarabu.

Kwa upande wa kusini, “ni hatari sana kukaribia kivuko cha Rafah, Ukanda wa Philadelphia, na pia maeneo yote ambayo vikosi vimepiga kambi huko Khan Younis,” jiji kuu katika sehemu ya kusini ya eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *