Nchini Senegal, kukamatwa tena kulifanywa katika msafara wa Rais wa zamani Macky Sall (2012-2024): Aliou Sall, kaka wa mkuu wa zamani wa nchi, na mkewe wamewekwa kizuizini jioni ya Alhamisi, Oktoba 9, kama sehemu ya uchunguzi uliofunguliwa na mamlaka iliyobobea katika kushughulikia kesi za uhalifu mkubwa wa kiuchumi na kifedha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Kufuatia ripoti ya shirika la kupambana na rushwa, CENTIF, ofisi ya mwendesha mashtaka wa fedha nchini Senegal imeamua kufungua uchunguzi wa kimahakama. Maswali yanahusiana na kuingia kwa pesa zinazochukuliwa na CENTIF kuwa ni zenye mashaka na ambazo zinaweza kujumuisha ufujaji wa pesa katika muktadha wa miamala ya ardhi.

Kulingana na wakili wa Aliou Sall, aliyewasiliana na RFI, fedha zilizohusika zilifikia faranga za CFA milioni 240 ambazo zilifika katika akaunti ya kampuni ya mali isiyohamishika ya meya wa zamani wa wilaya ya Guediawaye. Aliou Sall alitakiwa kutoa sababu ya asili ya pesa hizo wakati alipokuwa akisikilizwa.

Vibali kadhaa vinavyolenga washiriki wa karibu wa Macky Sall

Kukamatwa kwa Aliou Sall kunakuja huku kukiwa na kuharakishwa kwa taratibu za kisheria katika ofisi ya mashitaka ya fedha, kufuatia uhamisho wa baadhi ya faili arobaini na CENTIF, huku vibali kadhaa vikilenga washirika wa karibu wa Macky Sall.

Amadou Sall, mtoto wa kiume, anakabiliwa na chunguzi kadhaa kuhusu mtiririko wa fedha unaotiliwa shaka katika makampuni yanayohusishwa na familia yake. Lakini pia kuna mkuu wa vyombo vya habari na mshauri wa rais wa zamani, Madiambal Diagne: chini ya hati ya kimataifa ya kukamatwa, mahakama ya Seegal inataka kumhoji katika kashfa ya mamilioni ya fedha inayokadiriwa kuwa zaidi ya euro milioni 32.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *