Changamoto za afya ya akili imekuwa ikiongezeka siku hadi siku katika jamii zetu. Hii inatokana na baadhi yatu kubeba mizigo ya kihisia kwa muda mrefu bila msaada, jambo linaloathiri mahusiano, kazi, na hata afya ya mwili.

Wataalam wa afya wanasema hii imekuwa ikiongezeka kutokana na kasi ya maisha, changamoto za kiuchumi, na upungufu wa nafasi za kupata msaada wa kisaikolojia.

Tukitambua kwamba afya ya akili ni sehemu muhimu ya ustawi wa kila binadamu, je unachukua hatua zipi kudhibiti changamoto za afya ya akili katika maisha yako ya kila siku? Tuandikie maoni yako na tutayasoma #AdhuhuriLive saa 7:00 #UTV

#AzamTVupdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *